SANAA YA LUGHA

POEMS, STORIES, COMMENTS, NA KADHALIKA

2011 in review

Posted by Tabu Bin Tabu on January 1, 2012

The WordPress.com stats helper monkeys prepared a 2011 annual report for this blog.

Here’s an excerpt:

A San Francisco cable car holds 60 people. This blog was viewed about 2,200 times in 2011. If it were a cable car, it would take about 37 trips to carry that many people.

Click here to see the complete report.

Posted in Uncategorized | Leave a Comment »

MWENYE MATUSI

Posted by Tabu Bin Tabu on November 10, 2011

Yako majina ya vitu, mengine yasiyotajwa,

Yashangaza kuna watu, wenye uovu kujawa,

Waona kuwa si kitu, ni kama wanaolipwa,

Thawabu yako motoni, sikia mwenye matusi.

 

Mtu sio hayawani, anatumia akili,

Kuboboka hadharani, huwa ni kwake katili,

Matusi siwe kinywani, kama lusu tafadhali,

Thawabu yako motoni, sikia mwenye matusi.

 

Mdomo wako ni moto, wewe mja nakwambiya,

Wanena mambo mazito, hutaki kuyawaziya,

Ulimi wako ufito, mwilini wateketeya,

Thawabu yako motoni, sikia mwenye matusi.

 

Katu hutokaa tuli, kwa kweli tumefahamu,

Wewe ni ndumakuwili, mdomo wako ni sumu,

Wafitini kwa ukali, na kuua kama pumu,

Thawabu yako motoni, sikia mwenye matusi.

 

Hauna wakati wako, na kazi kwako hauna,

Kinywani hauna mwiko, mpyaro unajivuna,

Pasipo masikitiko, sokoni hutukanana,

Thawabu yako motoni, sikua mwenye matusi.

 

Utamkacho laana, ulimi wako huchungi,

Na lusifa wafanana, u kama mvuta bangi,

Unaitana majina, visivyotajwa kwa wingi,

Thawabu yako motoni, sikia mwenye matusi.

 

© Tabu Bin Tabu

24-10-2011

Posted in Mashairi | Leave a Comment »

STATS

Posted by Tabu Bin Tabu on October 30, 2011

Thanks so much my readers. Achieving 3000 stats is impressive.

Posted in Uncategorized | Leave a Comment »

NIPE NAFASI MHARIRI

Posted by Tabu Bin Tabu on February 19, 2011

Nipe nafasi mhariri, mawazo yangu sikika,
Lipate kuwa dhahiri, neno lilokusudika,
Nikupe langu shairi, gazetini kuandika,
Nipe nafasi mhariri, nisomeke gazetini.

Nipe nafasi mhariri, gazetini kuandika,
Wasifu wa mshairi, Musa Mzenga kutundika,
Kuyatunga mashairi, mpaka nikaelimika,
Nipe nafasi mhariri, nisomeke gazetini.

Malenga huyo dhahiri, alojaziwa baraka,
Mtunzi wa mashairi, alojaziwa fanaka,
Sifa zake zanawiri, mahali pangu zafika,
Nipe nafasi mhariri, nisomeke gazetini.

Mwalimu alo mahiri, omondi nakukumbuka,
Ulonifunza shairi, sifa zako zatapaka,
Kagumo nitawasiri, njia yako kutandika,
Nipe nafasi mhariri, nisomeke gazetini.

Walimu wetu wazuri kwa lugha wanasifika,
Kwa njema zao nadhari, nyingi zinabubujika,
Kiswahili chanawiri, na tena chaimarika,
Nipe nafasi mhariri, nisomeke gazetini.

© Tabu Bin Tabu 1989

Posted in Mashairi | 4 Comments »

JOGOO HAWI JONGOO

Posted by Tabu Bin Tabu on November 21, 2010

JOGOO HAWI JONGOO

Majina yapo ya vitu, hata yakiwa vitate,
Havitafanana katu, japo majina uite,
Hata kishikwa na kutu, kumwogopea siate,
Jogoo hawi jongoo, huishi kuwa jogoo.

Jogoo umbile lake, wadudu kuwabugia,
Ukware kipawa chake, vitembe wakatagia,
Kuwika laana yake, kiburi kamuingia,
Jogoo hawi jongoo, huishi kuwa jogoo.

Hata mvua kimnyea, akawa kijikunyata,
Usije kumchezea, kidhani kifo kapata,
Jongoo kimjongea, kumchokoza tajuta,
Jogoo hawi jongoo, huishi kuwa jogoo.

Hata awe ni kipora, haachi kujishaua,
Punje zako tachakura, kikosa kuziepua,
Hatasahau majira, yake kujiamkua,
Jogoo hawi jongoo, huishi kuwa jogoo.

Ukimwona amelala, ataamka kukicha,
Hataisahau sala, muumba wake kumcha,
Hata nyoka akiwala, tawararua kwa kucha,
Jogoo hawi jongoo, huishi kuwa jogoo.

©Samuel Mwenda 2010
Ustadh Tabu Bin Tabu
Karama antuamuo, Laare

Posted in Mashairi | 1 Comment »

MAJI UKIYAVULIA

Posted by Tabu Bin Tabu on November 14, 2010

MAJI UKIYAVULIA,

Katiba tumepitisha, kwa moyo wetu mmoja,
Ingawa tumebakisha, tujiunge kwa pamoja,
Ukabila ukaisha, tuwe kikundi kimoja,
Maji ukiyavulia, huna budi kuyaoga.

Yaliyopita si ndwele, tuyagange ya waleo,
Akili zetu ni nywele, zitufikishe upeo,
Tupate kuenda mbele, ndipo tuwe kivutio,
Maji ukiyavulia, huna budi kuyaoga.

Maovu tuyamalize, yatuvutao kinyume,
Juhudi tuziongeze, ufisadi utuhame,
Katiba tutekeleze, wakataao tuzime,
Maji ukiyavulia, huna budi kuyaoga.

Tuwe na moyo wa utu, tuache uhayawani,
Inua michezo yetu, hadi huku mashinani,
Tuhifadhi na misitu, nchi isiwe jangwani,
Maji ukiyavulia, huna budi kuyaoga.

Tulinde mali ya umma, ni yao walipa kodi,
Tusifanyiwe hujuma, kunyofolewa miradi,
Tufurahie uzima, tusipandwe na madadi,
Maji ukiyavulia, huna budi kuyaoga.

Tuitetee elimu, yetu na vizawa vyetu,
Ujuzi we ni muhimu, kuzipata kazi zetu,
Wengine tuwaheshimu, ni wananchi wenzetu,
Maji ukiyavulia, huna budi kuyaoga.

Sipitali ziwe nyingi, kilimo kiimarishwe,
Uchumi uwe msingi, mapato yainuliwe,
Tupate kazi kwa wingi, barabara zitengezwe,
Maji ukiyavulia, huna budi kuyaoga.

©Samuel Mwenda 2010
Ustadh Tabu Bin Tabu
Karama Antuamuo, Laare

Posted in Mashairi | 2 Comments »

KIUMBE

Posted by Tabu Bin Tabu on November 11, 2010

KIUMBE
Kiumbe, una hadhi gani?
Kumbe, hujijui u nani?
Mjumbe, waringiya nini?
Ujumbe, wakuhusu nini?

Uimbe, wimbo wa wahuni,
Pombe, itakulaza chini,
Kijembe, tapigwa kwa kani,
Uvimbe, nundu mgongoni.

Jipambe, nguo za katani,
Pembe, zitie kichwani,
Utambe, jae duniani,
Vikembe, ujaze nyumbani.

Kiumbe, pasi kuwa jinni,
Kumbe, hutii maanani,
Mjimbe, ulitumwa duniani,
Ujumbe, wapate imani.

Uimbe, kwa Mungu na dini,
Pombe haitakuauni,
Kijembe, hawatakufitini,
Uvimbe, wondoke mwilini.

Jipambe, kwa neno na dini,
Pembe, ondoa kichwani,
Utambe, hata na mbinguni,
Vikembe, ni wa duniani.

Kiumbe, utafurahini,
Kumbe, ndiko ukingoni,
Mjumbe, kwako ni mbinguni,
Ujumbe, ni wa shukurani.

© Tabu Bin Tabu 2010
Samuel Mwenda
Karama Antuamuo, Laare.

Posted in Mashairi | Leave a Comment »

JIRANI

Posted by Tabu Bin Tabu on November 6, 2010

JIRANI
Jirani wataka nini, nikupe ukatulie,
Sione mi maskini, sikia uzingatie,
Hutosheki maishani, jaribu ufikirie,
Una pembe na mkia, situdanganye hauna.

Umesukuma mpaka, kuchukua shamba langu,
Meniacha nikimaka, moyo mejaa uchungu,
Maji yale ya masika, ukayelekeza kwangu,
Huna akili kichwani, situdanganye unazo.

Kawaacha ng’ombe wako, na mbuzi kwa shamba langu,
Wakala bila kimako, mimea nayo magugu,
Na yale majibwa koko, fanza choo nyasi yangu,
Hauna wema moyoni, situhadae unao.

Kapa sumu wangu kuku, kafa na kujiishia,
Watuma paka usiku, kula kilichosalia,
Zamani nilikushuku, mayai kuniibia,
Una miguu minne, sifikirie hauna.

Mpaka wangu na wewe, kapanda mikalitusi,
Shambani kwangu kusiwe, rutuba sipate sisi,
Kumbe mfaidi ndiwe, ukiringa na kutusi,
Hauna soni jamani, sijitie hamnazo.

Nikuuzie wataka, shamba langu unasema,
Askari wanishika, kumbe ndiwe kala njama,
Ni mimi unanisaka, unangamize mapema,
Huna adabu hakika, sisingizie unayo.

Shika utakula huu, kidhani utaniweza,
Hasara ingoje juu, taanguka kwenye giza,
Unajifanya mkuu, wangamia nakujiza,
Huna maisha mwenzangu, sifikirie unayo.

© Samuel Mwenda 2010
Ustadh Tabu Bin Tabu
Karama Antuamuo, Laare.

Posted in Mashairi | Leave a Comment »

USTADHI

Posted by Tabu Bin Tabu on October 3, 2010

USTADHI
Ustadhi mwawataja, walio nao ujuzi,
Waliovuka daraja, kuwa ndio wamaizi,
Mnawapiga pambaja, kwa wingi wa utukuzi,
Kiwa lugha na wenyewe,wengine wafanya nini?

Mwahesabu ustadhi, wa sasa na wasifika,
Watunzi walio hadhi, kumbini waliowika,
Walochopoa mahadhi, kwa ndimi zilizowaka,
Kiwa sisi hatu radhi, wenyewe twafanya nini?

Sibague kwa kutaja, walio wako wandani,
Katu usifanye hanja, na wengine kuwahini,
Kikimbilia natija, ukawaacha juani,
Kiwa kaua wagala, haki utawapa lini?

Kuwapa wote la haki, fanya vema utafiti,
Kama kinyongo hutaki, kuepuka afiriti,
Usiwe unadhihaki, ukifanya tashititi,
Kiwa si sisi wenyewe, kilicho chetu ni nini?

Situachie makombo, twataka kula kinofu,
Watambue wa kitambo, japo sio watukufu
Mchango wao wa pambo, siuchukue hafifu,
Kiwa hawana ujuzi, kipimo mizani gani?

Tungo zimesarifiwa, tangu enzi za Muyaka,
Na watunzi wasifiwa, wengi wasohesabika,
Na wengi wakarithishwa, ujuzi uso mipaka,
Kiwa wa kale hutaji, walotajika ni nani?

Lugha yetu Kiswahili, sote tunajivunia,
Kama huoni dalili, si jambo kupigania,
Twatetea kwa ukali, siambe tunatania
Kiwa sio yetu sisi, lugha hii ni ya nani?

©Samuel Mwenda 2010
Ustadh Tabu Bin Tabu
Karama Antuamuo, Laare

Posted in Mashairi | Leave a Comment »

UTENZI WA DUNIA P5

Posted by Tabu Bin Tabu on June 20, 2010

UTENZI WA DUNIA P5
Maisha ya duniani,
Yana heri na huzuni,
Yanahitaji makini,
Mja kuyazingatia.

Mja ni mali ya mungu,
Aliziumba na mbingu,
Akayapanga mawingu,
Watu kuyafaidia.

Maumbile uliumbwa,
Hata paka naye mbwa,
Na karima ukapambwa,
Uweze kujiishia.

Alikupenda kwa dhati,
Hata ukiwa katiti,
Kaondoa vizingiti,
Upate kujiishia,

Ni wengi walitamani,
Kuwa huku duniani,
Hawakutamakani,
Muumba aliwazuia.

Mamilioni walikaza,
Maisha wakiyaanza,
Wasiweze kujibanza,
Rai haikuanzia.

Mwenye uhai ni mungu,
Anaondoa ukungu,
Na kutengeza viungu,
Maisha yakaanzia.

Ndani ya tumbo la mama,
Ukaanzia uzima,
Ukilala kama ndama,
Mungu alikutilia.

Nani aweza kusema,
Hukuwekwa na karima,
Nani kakupa uzima,
Tumboni kakuumbia?

Ulikuwa kajilaza,
Bila lolote kuwaza,
Hupati wa kukujuza,
Ilivyo hii dunia.

Miezi tisa hakika,
Na haipiti dakika,
Meza hajaitandika,
Chakula kukutilia.

Unachotaka wapata,
Hata pasipo kuita,
Huhitajiki kung’ata,
Chochote wajipatia.

© Tabu Bin Tabu 2010

Posted in Mashairi | Leave a Comment »

 
Follow

Get every new post delivered to your Inbox.